1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Silaha zinazouzwa kimagendo Sahel zinatokea barani Afrika

15 Februari 2023

Umoja wa Mataifa umesema kuwa nchi za ukanda wa Sahel zinahitaji kufanya juhudi zaidi katika vita dhidi ya ulanguzi wa silaha, ambazo kwa kiasi kikubwa zinatoka katika maghala ya silaha ya mataifa ya Afrika.

https://p.dw.com/p/4NVaE
Südafrika Schießerei in Soweto
Picha: AP Photo/picture alliance

Ripoti iliyotolewa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa kuhusu Madawa ya Kulevya na Uhalifu - UNODC, inasema nyingi ya zilaha zinazouzwa kimagendo katika eneo la Afrika Magharibi zinatoka kwingineko barani humo. 

Shambulizi la kigaidi lawauwa watu 56 Niger

Ripoti hiyo imesema silaha nyingi zinaingizwa katika eneo hilo kutoka kwa majeshi ya nchi nyingine, iwe ni kupitia kukamatwa kwenye uwanja wa mapambano, kuporwa kwenye maghala ya silaha, au kununuliwa kutoka kwa wafisadi ndani ya jeshi.

Watu 18 wauwawa katika shambulio Sahel

UNODC inasema mara nyingi silaha hizo zinasafirishwa katika shehena ndogo ndogo, kwa mwendo mrefu na kuingizwa katika mipaka mingi.

Baadhi ya silaha zinazosambaa katika eneo la Sahel zilitokea Sierra Leone na Liberia.