1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Raia nchini Mali wapiga kura

11 Agosti 2013

Vituo vya kupigia kura vimefunguliwa nchini Mali leo Jumapili kwa ajili ya uchaguzi wa duru ya pili wa rais nchini humo, wakati waziri mkuu wa zamani Ibrahim Boubakar Keita akionekana kuwa mbele.

https://p.dw.com/p/19NYs
A man casts his ballot during Mali's presidential election in Lafiabougou in Bamako, July 28, 2013. Voters in Mali headed to the polls on Sunday in a presidential election it is hoped will provide a fresh start to a country divided by a coup and a war in its desert north. REUTERS/Adama Diarra (MALI - Tags: ELECTION POLITICS)
Uchaguzi wa rais nchini MaliPicha: Reuters

Keita , ambaye ni maarufu kama IBK, alishinda asilimia 39.34 za kura katika duru ya kwanza ya uchaguzi nchini Mali Julai mwaka huu, akifuatiwa na waziri wa zamani wa fedha Soumaila Cisse ambaye alipata asilimia 19.44 ya kura.

Waziri mkuu huyo wa zamani hadi sasa amepata kuidhinishwa na karibu wagombea wote walioshiriki katika uchaguzi wa duru ya kwanza , ambapo ana matumaini itatosha kumpa ushindi muhimu.

Duru ya pili

Keita mwenye umri wa miaka 68 na Cisse mwenye umri wa miaka 63, walishapambana hapo kabla katika uchaguzi wa rais wa mwaka 2002, ambapo Cisse alitokeza kuwa wa pili na Keita alishika nafasi ya tatu nyuma ya mshindi wa uchaguzi huo , Amadou Toumani Toure.

Ibrahim Boubacar Keita Presidential candidate Ibrahim Boubacar Keita speaks at a campaign rally in Bamako July 21, 2013. Mali is due to hold presidential elections on July 28. REUTERS/Joe Penney (MALI - Tags: ELECTIONS POLITICS)
Mgombea wa urais Ibrahim Boubacar KeitaPicha: Reuters/Joe Penney

Keita alishindwa tena dhidi ya Toure mwaka 2007 na alijiunga na wagombea wengine katika kupinga matokeo ya uchaguzi huo, lakini mahakama ilitupilia mbali pingamizi lao.

Uchaguzi huo ni muhimu ili kusaidia nchi hiyo masikini katika Afrika magharibi kumaliza kipindi cha kutokuwa na uthabiti wakati ikijaribu kujitoa kutoka katika mapinduzi ya kijeshi pamoja na mapambano ya makundi ya Kiislamu hali ambayo imesababisha Ufaransa kutuma vikosi vyake vya jeshi katika koloni lake hilo la zamani.

Titel: DW_Soumaila-Cisse1 und 2 Schlagworte: Bamako, Präsidentschaftswahl, Spitzenkandidat, Staatsstreich, Soumaïla Cissé, URD (Union pour la République et la Démocratie, Union für Republik und Demokratie) Wer hat das Bild gemacht/Fotograf?: Katrin Gänsler Wann wurde das Bild gemacht?: 29. Juli 2013 Wo wurde das Bild aufgenommen?: Bamako, Mali
Soumaila Cisse mshindi wa pili katika duru ya kwanza ya uchaguzi MaliPicha: DW/K.Gänsler

Ufaransa yaingilia kati

Ufaransa ilifanya operesheni ya kijeshi Januari mwaka huu kuwazuwia wapiganaji wa Kiislamu kutosonga mbele kuelekea katika mji mkuu wa nchi hiyo Bamako. Kiasi ya wanajeshi 3,200 kutoka Ufaransa wako bado nchini Mali pamoja na jeshi la Umoja wa Mataifa la kulinda amani.

Keita alikuwa mgombea pekee ambaye hakukosoa mapinduzi ya mwezi Machi mwaka 2012, na anafikiriwa kuwa anapendelewa na jeshi kushika madaraka ya nchi hiyo.

Titel: DW_ Bundeswehr-Mali4: Schlagworte: Bundeswehr, Mali, deutsche Soldaten, malische Soldaten Wer hat das Bild gemacht/Fotograf?: Katrin Gänsler Wann wurde das Bild gemacht?: 26. Juli 2013 Wo wurde das Bild aufgenommen?: Koulikoro, Mali
Wanajeshi wa Ufaransa na wa UN nchini MaliPicha: Katrin Gänsler

Wengi wa raia wa Mali wanasema kuwa matokeo yoyote yawayo wana imani kuwa uchaguzi utaleta amani na uthabiti katika taifa hilo lililokumbwa na mizozo.

Uchaguzi huo pia utasaidia kufungua misaada ya kimataifa yenye lengo la kuijenga upya Mali. Vituo vya uchaguzi vitafungwa saa mbili usiku na matokeo yanatarajiwa kutangazwa katika muda wa siku tano.

Mwandishi : Sekione Kitojo / dpae

Mhariri: Sudi Mnette