Putin ziarani Ghuba
6 Desemba 2023Ziara hiyo ya Putin inalenga kutafuta uungaji mkono katika Mashariki ya Kati kutoka kwa madola hayo mawili yanayozalisha mafuta kwa wingi duniani na ambayo ni washirika wa Marekani, wakati vita vyake na Ukraine vikiendelea.
Putin aliwasili Abu Dhabi na kulakiwa na kiongozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu, Mohammed bin Zayed.
Soma zaidi: Waziri wa nje wa Marekani Hillary Clinton ziarani katika Ghuba
Wakati wa mkutano na kiongozi huyo wa Umoja wa Falme za Kiarabu, Putin alisema kuwa uhusiano kati ya Urusi na Umoja huo uko katika kiwango cha juu ambacho hakijawahi kushuhudiwa.
Soma zaidi: Merkel ziarani Saudi Arabia
Putin alisifu uhusiano baina ya nchi hizo mbili na kuutaja kuwa wa kipekee kihistoria na wakati huo huo kumualika Zayed kuhudhuria mkutano wa kilele wa kundi la mataifa yanayoinukia kiuchumi la BRICS mwakani huko Kazan.