POTSDAM: Ushirikiano muhimu kuhifadhi mazingira
17 Machi 2007Matangazo
Waziri wa mazingira wa Ujerumani,Sigmar Gabriel ametoa wito wa kuwepo ushirikiano kati ya juhudi za kulinda mazingira na maendeleo ya kiuchumi. Waziri Gabriel alikuwa akizungumza mjini Potsdam, mashariki mwa Ujerumani,kwenye mkutano wa mawaziri wa mazingira wa nchi 8 tajiri zilizoendelea kiviwanda na madola 5 yanayoendelea.Amesema nchi zinazoendelea hasa zina wasi wasi kuwa maendeleo yake ya kiuchumi yatakwenda pole pole kwa sababu ya juhudi mpya za kuhifadhi mazingira.Kwa sababu hiyo ni lazima kutia maanani kuwa ulinzi wa mazingira uende sambamba na ukuaji wa kiuchumi aliongezea waziri Gabriel.