1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi DRC yavunja maandmano ya upinzani

15 Septemba 2021

Polisi katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wamesambaratisha maandamano ya muungano wa upinzani Lamuka, yalioitishwa kupinga kuwepo wanasiasa katika Tume Huru ya Uchaguzi (CENI)

https://p.dw.com/p/40MhZ
Demonstrationen gegen die Präsidentschaftspartei Union für Demokratie und sozialen Fortschritt (UDPS) in Kinshasa
Picha: Getty Images/AFP/A. Mpiana

Polisi walitumia gesi ya kutoa machozi ili kutawanya maandamano hayo kabla ya kuanza kwenye eneo la Pascal katika wilaya ya Masina mashariki mwa mji wa Kinshasa.

Martin Fayulu, kiongozi wa Lamuka alichukuliwa kwa nguvu kutoka ndani ya gari lake na polisi ambao waliongozana naye hadi mjini, hali iliyosababisha vurugu kutoka kwa wafuasi wake, walioanza kuwarushia mawe polisi. Waandamanaji kadhaa walikamatwa.

Muungano wa Lamuka unamshutumu Rais Félix Tshisekedi kwa kuweka wanasisa wake kwenye Tume Huru ya Kitaifa ya Uchaguzi kwa madai ya kusaidia kutoufanya uchaguzi mwaka 2023 pamoja na kutoa matokio ya udanganyifu.

Lamuka yasikitishwa na matukio ya polisi dhidi yao

DR Kongo Martin Fayulu in Kinshasa
Martin Fayulu, Kiongozi wa LamukaPicha: Reuters/B. Ratner

Baadhi ya polisi waliwawabughudhi waandishi wa hahabari, hadi kufikia kumkamata mwenzetu Patient Ligodi wa shirika la utangazaji la Ufaransa RFI, jambo ambalo msemaji wa jeshi la Polisi Kanali Pierrot Mwana Mputu ameomba radhi.

"Tunahuzunishwa na kukamatwa rafiki yetu mwandishi Patient wa RFI, Ila kamanda aliamuru aachiliwe haraka na arudishiwe vitu vyake, alisema Kanali Pierrot Mwana Mputu.

Muungano Lamuka umeelezea kusikitishwa na ukandamizaji dhidi ya maandamano yake wakati ulimwengu ukiadhimisha Siku kuu ya Kidemokrasia.

Mwnadishi: Jean Noël Ba-Mweze, DW,   Kinshasa.