1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Asili na mazingiraPapua New Guinea

Papua New Guinea yatangaza kususia mkutano wa COP29

31 Oktoba 2024

Serikali ya Papua New Guinea imetangaza kususia mkutano wa kilele wa Umoja wa Mataifa wa hali ya hewa COP29 unaotarajiwa kufanyika nchini Azerbaijan mwezi ujao.

https://p.dw.com/p/4mQyy
Papua New Guinea yatangaza kususia COP29
Papua New Guinea yatangaza kususia COP29Picha: Christiane Oelrich/dpa/picture alliance

Waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Justin Tkatchenko, ameliambia shirika la habari la AFP kwamba hakuna haja ya kuhudhuria mkutano huo kwa sababu hakuna linalotekelezwa.

Tkatchenko ameongeza kuwa wamechoshwa na maneno matupu ambayo hayajapata ufanisi wowote katika muda wa miaka mitatu iliyopita.

Waziri huyo pia amesema kuwa nchi yake ni ya tatu kwa kuwa na eneo kubwa la misitu ya Kitropiki na kwamba imeathirika kutokana na uchafuzi wa mazingira wa mataifa hayo makubwa na hakuna taifa linalowajibishwa.