1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Francis atetea kuwabariki wapenzi wa jinsia moja

26 Januari 2024

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis ametetea hatua ya hivi karibuni ya kanisa hilo kuidhinisha kuwabariki wapenzi wa jinsia moja.

https://p.dw.com/p/4bj5A
Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis.
Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis.Picha: Tiziana Fabi/AFP/Getty Images

Kiongozi huyo wa kidini hata hivyo ameweka wazi kuwa, kanisa limeidhinisha hatua ya kuwabariki wapenzi wa jinsia moja na wala sio ndoa kati ya wapenzi wa jinsia moja.

Mnamo mwezi Desemba, Idara ya Mafundisho ya Kanisa Katoliki, ilisema makasisi wanaweza kuwabariki watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja kwa kuzingatia mazingira fulani maalum.

Soma zaidi: Papa aridhia kubariki mahusiano ya jinsia moja yasiofanana na ndoa

Hatua hiyo ya kanisa ilizusha ukosoaji mkubwa hasa barani Afrika huku wakosoaji wakilishutumu kanisa kwa kubadili msimamo wake wa awali kuhusu ndoa za wapenzi wa jinsia moja na ushoga, ambao unapingwa na kanisa.

Upinzani dhidi uamuzi wa Vatican umekuwa mkubwa hasa nchini Malawi, Nigeria, Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.