Wanaharakati wapongeza kuwabatiza waliobadili jinsia
11 Novemba 2023Miongoni mwa waliosifu hatua hiyo ni kasisi wa tawi la kijesuti ambalo ni sehemu ya kanisa katoliki James Martin pamoja mchungaji Jean-Michel Dunand ambaye ni mwanzilishi wa kanisa linalotoa huduma kwa watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.
Soma zaidi: Papa ashutumu ushoga kufanywa uhalifu
Wawili hao wamesema muongozo wa Vatican wa kuruhusu kubatizwa kwa watu waliobadili jinsia, wale wanaolelewa na wapenzi wa jinsia moja au watoto waliozaliwa na mwanamke aliyebeba mimba kwa niba ya mtu mwingine ni hatua moja mbele kuelekea ujumuishi ndani ya kanisa katoliki.
Kwenye waraka uliochapishwa siku ya Jumatano na kuidhinishwa na Papa Francis, kanisa limeridhia kubatizwa kwa watu hao lakini kwa tahadhari kwamba zoezi hilo halitazusha kashfa au mivutano.