Papa Francis aiomba Urusi irudi kwenye makubaliano ya nafaka
30 Julai 2023Matangazo
Karibu tani milioni 33 za nafaka zilisafirishwa kutoka katika bandari za Ukraine chini ya makubaliano hayo yaliyofikiwa mwaka uliopita, na kupunguza gharama na kitisho cha upungufu wa chakula duniani.
Papa Francis ametoa wito huo katika sala ya Jumapili, akiiomba Urusi kurudi kwenye makubaliano.
Soma zaidi: Papa arejea wito wa kustishwa mapigano Ukraine
Amesema wakati wote wamekuwa wakiwaombea mashahidi wa Ukraine, ambako vita vinaharibu kila kitu, ikiwa ni pamoja na nafaka, akisema ni kosa kubwa mbele za Mungu kwa kuwa nafaka ni zawadi kutoka kwake kwa ajili ya kuwalisha wanadamu.
Urusi imejiondoa kwenye makubaliano hayo wiki mbili zilizopita na imekataa kuongeza muda wake.