1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Oslo. Kiongozi wa mpango wa mazingira kujiuzulu.

6 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEdp

Klauf Toepfer, kiongozi wa mpango wa umoja wa mataifa wa mazingira, anapanga kujiuzulu kutoka wadhifa huo baada ya kukataa kuongeza muda wa kazi yake ambayo ameishikilia kwa muda wa miaka nane.

Mpango huo wa umoja wa mataifa wa mazingira umesema leo kuwa Bwana Toepfer mwenye umri wa miaka 67 ameamua kutoongeza muda wa miaka miwili katika mpango huo wenye makao yake makuu mjini Nairobi Kenya , kazi aliyopewa na katibu mkuu wa umoja wa mataifa Kofi Annan .

Bwana Toepfer alikuwa waziri wa mazingira wa Ujerumani kutoka mwaka 1987-94 katika serikali iliyokuwa ikiongozwa na chama cha Christian Democrats.