1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ofisi za Al Jazeera mjini Ramallah zafungwa kwa siku 45

Sylvia Mwehozi
22 Septemba 2024

Ofisi za kituo cha utangazaji cha Al Jazeera katika eneo linalokaliwa la Ukingo wa Magharibi,katika mamlaka ya Wapalestina, zimevamiwa leo na kuamriwa kufungwa kwa siku 45.

https://p.dw.com/p/4kwnp
Askari wa Israel akiwa amesimama karibu na gari la jeshi karibu na ofisi za Al-Jazeera
Askari wa Israel akiwa amesimama karibu na gari la jeshi karibu na ofisi za Al-JazeeraPicha: Mohamad Torokman/REUTERS

Ofisi za kituo cha utangazaji cha Al Jazeera katika eneo linalokaliwa la Ukingo wa Magharibi,katika mamlaka ya Wapalestina, zimevamiwa leo na kuamriwa kufungwa kwa siku 45. Al Jazeera imeripoti kwamba wanajeshi wa Israel waliokuwa na silaha na kuficha nyuso zao walivamia ofisi za kituo hicho mjini Ramallah na kukabidhi amri ya kufungwa ofisi kwa mkuu wa kituo Walid al-Omari mapema leo Jumapili.

Soma: Al Jazeera yataka ICC ichunguze mauaji ya mwandishi Akleh

Mnamo mwezi Mei, serikali ya Israel ilifunga shughuli zaAl Jazeeranchini humo baada ya kupitishwa kwa sheria ya vyombo vya habari inayotoa mamlaka kwa serikali kuvipiga marufuku vituo vya utangazaji wa kigeni, endapo vitaonekana kuhatarisha usalama wa nchi. Ofisi za Al Jazeera zilifungwa, vifaa kukamatwa na kituo hicho kuondolewa katika mawasiliano ya satelaiti na wavuti kuzuiliwa.