1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaQatar

Al Jazeera yataka ICC ichunguze mauaji ya mwandishi Akleh

6 Desemba 2022

Kituo cha habari cha kimataifa cha Al Jazeera kimepeleka ombi rasmi kwa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC kuchunguza mauaji yaliyotokana na kupigwa risasi mwandishi habari wake Shireen Abu Akleh.

https://p.dw.com/p/4KYdH
Berlin | Gedenk-Graffiti für die in Jenin getötete palästinensische Journalistin Shireen Abu Akleh
Picha: Christoph Strack/DW

Kituo cha Aljazeera kimeishutumu serikali ya Israel kwa kuwalenga hususan waandishi wake  na kukiita kifo cha Abu Akleh kuwa uhalifu wa kivita.

Kituo hicho cha habari kimemtaka mwendesha mashtaka wa ICC Karim Khan kujumuisha mauaji ya mwandishi habari huyo na mashambulizi ya anga ya jeshi la Israel mwaka jana dhidi ya ofisi za Al Jazeera katika Ukanda wa Gaza katika uchunguzi wake unaoendelea kuhusu madai ya kutokea uhalifu wa kivita katika Ukingo wa Magharibi na Gaza.

Kufuatia shinikizo za kimataifa, jeshi la ulinzi la Israel lilikiri huenda mmoja wa wanajeshi wake alimpiga risasi mwandishi huyo maarufu lakini lilikanusha tukio hilo lilikuwa la makusudi na kuifunga kesi hiyo.