Noumea, New Caledonia. Uchafuzi wa mazingira wasababisha vifo vya mamilioni ya watu.
23 Septemba 2005Shirika la afya duniani WHO limesema kuwa uchafuzi wa hali ya hewa pamoja na kuharibika kwa mazingira unaua watu milioni moja kila mwaka katika eneo la bara la Asia linalopakana na bahari ya Pacific.
Maafisa wa WHO, wanaofanya mkutano wao wa eneo mjini Noumea, New Caledonia , wamehusisha hali hiyo na uchafu unaotoka viwandani pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa.
Licha ya kuwa ufumbuzi wa kiteknolojia kama vifaa vya kusafisha maji vinapatikana , wataalamu hao wamesema kuwa nchi nyingi masikini hazina uwezo wa kuvunja uhusiano kati ya uchafuzi huo wa mazingira na hali mbaya ya kiafya ya wananchi wao inayoendelea kuongezeka. Shirika hilo la afya ulimwenguni WHO inapendekeza juhudi za pamoja zichukuliwe ili kuweza kupambana na matatizo hayo katika maeneo mbali mbali.