Nigeria yawaonya raia wake dhidi ya kusafiri kuelekea China
30 Januari 2020Matangazo
Kulingana na waziri wa afya wa nchi hiyo Osagie Ehanire wale wanaorudi Nigeria kutoka China pia wanastahili kujiweka karantini wenyewe kwa kipindi hicho hicho cha wiki mbili.
Ehanire amedai wanaoonyesha dalili za virusi hivyo ndio watakaowekwa katika karantini ya lazima hospitali.
Virusi hivyo ambavyo kitovu chake ni mji wa Wuhan huko China kimesababisha vifo vya watu 170 na visa vya virusi hivyo vikiripotiwa katika nchi nyengine duniani pia.
Hakujathibitishwa kisa chochote cha virusi hivyo barani Afrika ingawa maafisa wa Sudan wameripoti kuwa wameripoti kuhusu watu wawili wanaoshukiwa kuambukizwa.