New York:Makampuni yatetea hifadhi ya mazingira
21 Februari 2007Kundi la makampuni 85 ya kibiashara duniani, limetoa wito wa hatua za haraka kupambana na ongezeko la ujoto duniani. Makampuni hayo yakiwemo lile la ndege la ufaransa-Air France na kampuni ya bima ya Ujerumani-Allianz, yanasema yataanzisha aina mpya ya ufundi ili kupunguza utoaji na matumizi ya gesi zinazochafua mazingira na kusababisha ongezeko la ujoto duniani, lakini yameongeza kwamba serikali hazina budi kuwa na utaratibu wa kisayansi juu ya malengo yanayokusudiwa katika kupunguza utoaji wa gesi hizo.
Wakuu wa makampuni hayo makubwa ya kibiashara wanakutana katika chuo kikuu cha Columbia nchini Marekani wamezitaka serikali duniani zitoze gharama maalumu kuhusu utoaji wa gesi chafu ya Carbon dioxide ambayo ni sehemu kubwa ya uchafuzi wa mazingira. Hatua kama hiyo inapigiwa upatu pia na Umoja wa ulaya.