1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK : Makubaliano ya mazingira yamekwenda kombo

13 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC2e

Umoja wa Ulaya umesababisha mkorogo mwishoni mwa mkutano wa wiki mbili wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo Endelevu ambacho ni chombo kikuu cha Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kulinda mazingira.

Waziri wa mazingira wa Ujerumani Sigmar Gabriel ambaye anayawakilisha mataifa yote ya Umoja wa Ulaya chini ya urais wa Ujerumani wa umoja huo pamoja na Kamishna wa Mazingira wa Umoja wa Ulaya Stavros Dimas wamegoma kusaini waraka wa mwisho kwa kusema kwamba umeshindwa kujifunga vya kutosha na ahadi za malengo ya kulinda mazingira na nishati.

Wametowa hoja kwamba makubaliano hayo yameshindwa kuzingatia ahadi zilizopita za kutunza mazingira.