1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New York. Leo ni siku ya mazingira. Miji yatakiwa kupanda miti zaidi.

5 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF6j

Siku ya mazingira duniani inaadhimishwa leo, kwa matukio ya matumizi ya vitu vilivyokwisha tumika na kufanya usafi, pamoja na miito ya kuifanya miji hapa duniani ambayo inazidi kupanuka kuwa safi na iliyopandwa miti.

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Bwana Kofi Annan amesema kuwa mmoja kati ya kila watu watatu wanaoishi mjini wanaishi katika vibanda poromoka, mara nyingi wakikosa maji safi na huduma ya ukusanyaji wa taka.

Viongozi wa zaidi ya miji 50 mikubwa duniani wanapanga kutia saini mjini Francisco mpango utakaotoa viwango vipya kwa ajili ya mipango bora ya miji, ikiwa ni pamoja na kuboresha mfumo wa usafiri wa jamii.

Mkuu wa shirika la ulinzi wa mazingira la umoja wa mataifa Bwana Klaus Topfer amesema kuwa miji ni mzigo mkubwa katika mali asili za dunia na inachangia katika kuchafua mazingira.

Kitabu cha picha za satalite kilichochapishwa na kutolewa umoja wa mataifa siku ya ijumaa kinaonesha misitu inavyoharibiwa, maeneo ya barafu yanavyoyeyuka, bahari zinavyokauka na uchafuzi wa maji katika mito na mabwawa.