Netanyahu avunja Baraza lake la vita nchini Israel
17 Juni 2024Gantz alijiondoa katika baraza hilo, akidai Netanyahu ameshindwa kuwa na mpango maalum juu ya vita vya Gaza.
Netanyahu sasa anatarajiwa kuwa na majadiliano kuhusu vita hivyo na kundi dogo la mawaziri akiwemo waziri wa Ulinzi Yoav Gallant, na waziri wa masuala ya kimkakati Ron Dermer aliyekuwa katika Baraza hilo.
Soma pia:Mpango wa usitishaji vita Gaza kuamua hatma ya kisiasa ya Netanyahu
Waziri Mkuu huyo wa Israel amekuwa akipata shinikizo kutoka kwa washirika wake wa chama chenye misimamo mikali ya kidini katika muungano wake kutoka kwa waziri wa fedha Bezalel Smotrich Waziri wa usalama wa kitaifa Itamar Ben-Gvir, waliotaka kujumuishwa katika Baraza la vita la Israel, hatua ambayo ingeleta mvutano na washirika wake wa kimataifa akiwemo Marekani.