Ndege iliyowabeba Mawaziri wa Ujerumani yapata tatizo
13 Aprili 2023Matangazo
Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Boris Pistorius na mwenzake wa maendeleo Svenja Schulze wamewasili mjini Niamey kuanza ziara ya siku kadhaa katika eneo la Sahel.
Msemaji wa wizara ya ulinzi ameliambia shirika la habari la Ujerumani dpa kwamba, ndege ya kijeshi ya Ujerumani iliyowasafirisha bado inaweza kutumika lakini licha ya tatizo hilo.
Katika ziara hiyo ambayo haikutangazwa kabla kwa sababu za kiusalama , mawaziri wote wawili wanataka kujionea hali ilivyo katika eneo hilo kabla jeshi la Ujerumani, Bundeswehr, halijaondoka nchini Mali.
Serikali ya Ujerumani inapanga kuwaondoa zaidi ya wanajeshi wake elfu moja walio chini ya mpango wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa MINUSMA ifikiapo Mei mwaka ujao wa 2024.