1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NATO:Lazima Ukraine ipate silaha zaidi

14 Februari 2023

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya kujihami NATO Jens Stoltenberg amerejelea tena tamko lake leo Jumanne kwamba, Jumuiya hiyo ni lazima ihakikishe Ukraine inapata silaha inazohitaji kushinda vita vyake na Urusi.

https://p.dw.com/p/4NSDf
Belgien | Treffen der Nato-Verteidigungsminister in Brüssel
Picha: Johanna Geron/REUTERS

Stoltenberg amesema ni wazi kwamba Rais wa Urusi Vladimir Putin hajiandai kwa makubaliano ya amani na jirani yake, lakini anaendelea na matayarisho ya kufanya mashambulizi zaidi. 

Soma pia:NATO yaonya juu ya uhaba wa risasi Ukraine

Urusi inadaiwa kuendeleza mashambulizi makali katika mji wa Bakhmut siku kadhaa kabla ya uvamizi wake nchini Ukraine kutimiza mwaka mmoja.

Maafisa wa Ukraine wamesema wanajeshi wake wanapambana na wanajeshi wa Urusi katika mashambulizi hayo ya ardhini mashariki mwa taifa hilo.