NATO:Wakati wa kuridhia Finland na Sweden kujiunga
16 Februari 2023Matangazo
Stoltneberg alikuwa akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari pamoja na waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu.
Cavusoglu hata hivyo amerudia msimamo wa Uturuki kwambahawatayatathmini maombi hayo kwa pamoja, na hasa kufuatia mvutano ulioibuka mwezi uliopita, baada ya tukio la kuchomwa Qur'an nje ya ubalozi wa Ankara mjini Stockholm.
Soma pia:NATO yajadili kuongeza kiwango cha matumizi ya ulinzi
Finland na Sweden waliomba kujiunga na NATO baada ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine mwezi Februari mwaka jana, lakini Hungary na Uturukibado hawajaidhinisha hadi sasa.