1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NATO kuchunguza madai ya mauaji wa raia Libya

Thelma Mwadzaya1 Aprili 2011

Jumuiya ya Kujihami ya NATO inayachunguza madai yaliyotolewa na askofu mmoja wa kikatoliki raia wa Italia kuwa kiasi ya watu 40 wanaripotiwa waliuawa katika shambulio la bomu lililotokea kwenye mji mkuu wa Tripoli.

https://p.dw.com/p/10lgP
Waasi wanaopigana LibyaPicha: dapd

 Kulingana na maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, dhamira ya operesheni ya kijeshi inayoendelea Libya ni kuwalinda raia wa kawaida. Itakumbukwa kuwa Jumuiya ya Kujihami ya NATO ilichukua hapo jana Alhamisi, usukani wa kuisimamia operesheni hiyo. Wakati huohuo, uongozi wa Uingereza unamhoji Waziri wa mambo ya nje wa Libya,  Moussa Koussa, aliyekimbilia huko kutafuta hifadhi baada ya kuasi na kujiuzulu.

Mwanadiplomasia huyo amesisitiza kuwa Moussa Koussa anazungumza na maafisa wa serikali ya Uingereza kwa hiari na kwamba hajapewa kinga yoyote.Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Uingereza ,David Cameron, amesema kuwa kitendo hicho cha Moussa Koussa kuasi ni pigo kubwa kwa uongozi wa Kanali Muammar Gaddafi.

Kanada schickt CF-18-Kampflugzeuge wegen Libyen nach Europa
Ndege za vita za kigeni kwenye operesheni ya Odyssey New DawnPicha: picture-alliance/dpa/Department of National Defence

Wakati huohuo,Waziri wa Ulinzi wa Marekani , Bill Gates, ameirejelea tena kauli iliyotolewa na Rais Obama kuwa hakuna wanajeshi wowote wan chi kavu watakaoingia kwenye ardhi ya Libya.Hata hivyo waziri huyo aliepuka kuzielezea taarifa zilizotangazwa na vyombo vya habari kuwa maafisa wa shirika la ujasusi la Marekani la CIA wamekuwa nchini Libya kwa wiki kadhaa.