1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mtoto wa Biden akutwa na hatia kwa kesi ya bunduki

12 Juni 2024

Mahakama nchini Marekani imemtia hatiani, Hunter Biden kwa makosa yaliohusu umiliki wa bunduki ya ikiwa ni kesi ya kwanza ya jinai ya kihistoria kumkabili mtoto wa rais aliye madarakani.

https://p.dw.com/p/4gvwa
MarekaniI Hunter Biden
Hunter Biden, 54, anashutumiwa kwa kusema uwongo kuhusu matumizi yake haramu ya dawa za kulevya aliponunua bunduki mwaka wa 2018.Picha: Ryan Collerd/AFP

Mtoto wa kiume wa Rais Joe Biden mwenye umri wa miaka 54 alipatikana na hatia kwa makosa yote matatu ya uhalifu yaliyotokana na ununuzi wake wa bunduki mwaka 2018 akiwa mwathirika wa madawa ya kulevya aina ya cocaine. Uamuzi huo unakuja wakati baba yake yupo katika harakati za kuwania tena urais, na kufuatia uamuzi huo Rais Biden mwenyewe kabadilisha ratiba yake na kufanya safari ya kwenda Wilmington, Delaware, mji wa familia yake ambapo kesi hiyo iliikuwa ikisikilizwa.Taarifa iliyotolewa muda mfupi baada ya kutolewa uamuzi huo Biden alionesha upendo na mshikamano kwa mtoto wake. Anaweza kukabiliwa na kifungo cha hadi miaka 25 jela, ingawa kutokana na makosa yanayomkabili na kama mkosaji wa mara ya kwanza muda wa kifungo sijambo linalotazamiwa.