Hunter Biden afutiwa kesi ya kumiliki silaha
12 Oktoba 2023Suala la kumiliki silaha ambalo lilikuwa sehemu ya makubaliano ya kukubali makosa yaliyovunjika kwenye kesi inayomkabili mtoto wa kiume wa Rais Joe Biden wa Marekani aitwaye Hunter Biden, limefutwa baada ya jaji wa kesi hiyo kulikataa ombi la waendesha mashitaka.
Amri ya Jaji Maryellen Noreika imeliondowa rasmi shitaka hilo na sasa nafasi yake inachukuliwa na kosa la dharau.
Mtoto huyo wa Rais Biden anashitakiwa kwa kuvunja masharti yanayowazuwia watumiaji madawa ya kulevya kumiliki silaha, baada ya kununua na kubakia na bastola moja kwa siku 11 mnamo mwaka 2018, kipindi ambacho alikuwa mtumiaji wa madawa hayo.
Mapema mwezi huu alikanusha kutenda kosa, wakati kesi hiyo ikielekea kutolewa hukumu yake huku uchaguzi wa mwaka 2024, ambapo baba yake anawania kutetea kiti chake ukiwadia.