Mkutano wa mazingira mjini Nairobi
16 Novemba 2006Nairobi
Mkutano wa kimataifa kuhusu hali ya hewa mjini Nairobi umeingia katika awamu muhimu wiki hii.Akihutubia mkutano huo hapo jana,katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Kofi Annan alikosoa ile hali ya kutowajibika vya kutosha baadhi ya mataifa.Amesema kunakosekana moyo wa kutaka kushika usukani katika suala la kuhifadhiwa mazingira.Waziri wa mazingira wa serikali kuu ya Ujerumani Sigmar Gabriel ameshadidia mchango wa Ujerumani katika usafi wa mazingira.Ametoa mwito hata hivyo ulimwengu mzima uwajibike .Waziri wa mazingira wa serikali kuu ya Ujerumani Sigma Gabriel ametilia mkazo haja ya kujumuishwa India na jamhuri ya umma wa China katika juhudi za kulinda mazingira.Amesema wakati huo pengine Marekani pia itawajibika. Mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa utamalizika kesho mjini Nairobi.