Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa waanza
19 Septemba 2023Akizungumza kabla ya mkutano huo wa kila mwaka, ambao unawakutanisha marais, mawaziri wakuu na wafalme, Guterres alisema watu wanatarajia viongozi wao watafute njia ya kukabiliana na mizozo inayoikumba dunia.
Guterres alisema ulimwengu unahitaji hatua zichukuliwe na sio maneno matupu katika kukabiliana na "hali ya dharura ya mabadiliko ya tabianchi, migogoro inayoongezeka, matatizo makubwa ya kiteknolojia na kupanda kwa gharama za maisha duniani ambazo zinaongeza njaa na umasikini."
Soma zaidi: AU kujadili unachama wa Mali, Burkina Faso na Guinea
Umoja wa Mataifa kuijadili Libya
Guterres alisema mkutano huo ungetawaliwa na mijadala kama vile vita, mabadiliko ya tabianchi na ukosefu wa usawa.
Viongozi wengine waliotarajiwa kuhutubia kwenye mkutano huo siku ya Jumanne (Septemba 19) ni kutoka Marekani, Brazil, Uturuki, Ukraine, Japan na Iran.