1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Misri, Sudan na Ethiopia zajadili bwawa linalozozaniwa

2 Desemba 2019

Misri ni mwenyeji wa duru mpya ya mazungumzo na Ethiopia na Sudan juu ya bwawa linalozozaniwa, ambalo limejengwa na Ethiopia katika mto Nile.

https://p.dw.com/p/3U6UK
Deutschland Compact with Africa Initiative in Berlin | Agyptischer Präsident al-Sissi
Picha: picture-alliance/AFP/J. Macdougall

Mazungumzo haya mapya ni sehemu ya makubaliano yaliyofikiwa jijini Washington mwezi uliopita ya kumaliza mzozo wa muda mrefu juu ya matumizi ya mto huo.

Mawaziri wa maji wa Misri, Ethiopia na Sudan wanakutana leo na kesho kwa ajili ya mazungumzo ya kanuni za uendeshaji wa bwawa kubwa la umeme.

Ethiopia ilianza ujenzi wa bwawa hilo la dola bilioni 4.8 mwaka 2010, ikijaribu kuwa muuzaji mkubwa wa nishati ya umeme barani Afrika.

Misri inategemea zaidi maji ya mto Nile kuendesha sekta ya kilimo, viwanda na matumizi ya maji ya majumbani, huku ikohofia kuwa bwawa hilo litaathiri usambazaji wake. Hata hivyo Ethiopia inasema madai ya Misri hayana misingi.

Misri inakuwa mwenyeji wa mazungumzo hayo ya duru ya pili kati ya duru nne zilizokubaliwa mjini Washington mwezi Novemba.