1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merkel: Masharti magumu ni muhimu kudhititi COVID19

16 Aprili 2021

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amewahimiza wabunge nchini humo kuridhia mamlaka mapya yatakayomruhusu kulazimisha vizuwizi na amri za kutotoka nje usiku katika maeneo yenye viwango vikubwa vya maambukizi

https://p.dw.com/p/3s7SS
Deutschland Bundeskanzlerin Angela Merkel (CDU)
Picha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Angela Merkel amesema Wajerumani wengi wanaunga mkono hatua kali zaidi ili kuvishinda virusi vya corona. 

Serikali ya Merkel inalitaka bunge kubadili sheria ya Ulinzi dhidi ya Maambukizi ili kuziwezesha mamlaka za shirikisho kuweka vikwazo hata kama viongozi wa majimbo watazipinga akitumai kupunguza shinikizo katika vyumba vya wagonjwa mahututi.

soma zaidi: Ujerumani kuweka sheria ya kitaifa kudhibiti COVID-19

Uwekaji wa amri za kutotoka usiku na kuipa serikali kuu mamlaka ya kuzitekeleza katika majimbo 16 ya Ujerumani umezusha ukosoaji pia kutoka ndani ya muungano wa vyama vya Merkel ambao uchunguzi wa maoni unaonesha utapata matokeo mabaya zaidi katika uchaguzi mkuu wa mwezi Septemba.