Meli ya Ocean Viking yawaokoa wahamiaji zaidi ya 600
12 Agosti 2023Takwimu hizo zinaashiria ongezeko jipya la idadi ya watu wanaofanya safari hatari kujaribu kuingia Ulaya.
Soma zaidi: Italia kuwa mwenyeji wa mkutano wenye lengo la kupunguza wimbi la wahamiaji
Shirika linaloendesha meli hiyo la SOS Méditerranée limesema wengi wa waliookolewa walikuwa safarini kutoka mji wa mwambao wa Italia wa Sfax wakielkea kisawa cha Lampedusa nchini Italia.
Soma zaidi: Wahamiaji zaidi ya 900 wafa maji pwani ya Tunisia
Kulingana na shirika hilo jumla ya watu 623 waliokuwa wakisafiri kwa kutumia boti hatari za mpira wamepatiwa msaada na sasa wamo kwenye meli ya Ocean Viking na wanatarajiwa kufikishwa kwenye bandari za Italia baadaye leo.
Wahamiaji hao ni kutoka mataifa ya Sudan, Guinea, Burkina Faso, Ivory Coast, Benin na Bangladesh. Uokoaji huo umefanyika kiasi wiki moja tangu kutokea vifo vya makumi ya wahamiaji baada ya boti kadhaa kuzama baharini zikiwa njiani kuelekea mataifa ya Ulaya.