Wahamiaji zaidi ya 900 wafa maji pwani ya Tunisia
27 Julai 2023Feki ameliambia bunge la nchi yake kuwa miongoni mwa maiti hizo, 36 zilikuwa za raia wa Tunisia na 267 za wahamiaji wa kigeni, huku waliobakia bado uraia wao haujatambuliwa.
Tunisia imechukua nafasi ya Libya kama kituo kikuu cha kanda hiyo kwa watu wanaokimbia umasikini na mizozo Afrika na Mashariki ya Kati kwa matumaini ya kwenda Ulaya kupata maisha bora.
Soma zaidi: Mpango wa EU wa kuokoa uchumi wa Tunisia
Boti nyingi zenye wahamiaji zinaondoka kwenye pwani ya mji wa kusini wa Sfax.
Takwimu rasmi zinaonesha kuwa takribani wahamiaji 75,065 waliwasili nchini Italia baina ya Januari hadi katikati ya mwezi Julai mwaka huu, ikilinganishwa na wahamiaji 31,920 katika miezi sawa na hiyo kwa mwaka jana.
Zaidi ya nusu ya wahamiaji hao waliondokea nchini Tunisia.