SiasaUkraine
Mawaziri wa nje wa Ulaya waonyesha mshikamano na Ukraine
2 Oktoba 2023Matangazo
Mkuu huyo wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell aidha amesema mustakabali wa Ukraine upo mikononi mwa Umoja huo wa Ulaya.
Huo ni mkutano wa kwanza wa ngazi ya mawaziri kufanyika kwenye ardhi ya nchi isiyo mwanachama wa Umoja wa Ulaya.
Waziri wa masuala ya kigeni wa Ukraine Dmytro Kuleba amesema mkutano huo unatuma ujumbe kwamba Umoja wa Ulaya unatanuka kuingia Ukraine. Mkutano huo haukutangazwa hapo kabla kutokana na sababu za kiusalama.
Moja ya ajenda ya majadiliano ni pendekezo la Borrell, la kurefusha muda wa kujitolea kuifadhili Ukraine kwa kuipa silaha na pia kutumia fedha za Umoja wa Ulaya kutoa ndege za kisasa za kivita na makombora kwa Ukraine.