Mawaziri wa ndani wa Umoja wa Ulaya wanakutana Brussels
5 Desemba 2023Kamishna wa mambo ya ndani katika Umoja wa Ulaya Ylva Johansson akiwasili kwenye mkutano huo, amesema Ulaya kwa hivi sasa inashuhudia ongezeko la kitisho cha ugaidi kufuatia vita vinavyoendelea Gaza. Amesema mgogoro huo kati ya Israel na Hamas umesababisha mkwamo katika nchi za Umoja waUlaya na katika msimu ujao wa mapumziko, kuna kitisho kikubwa cha kutokea mashambulizi ya kigaidi katika nchi za umoja huo. Ametangaza hatua ya kutoa yuro milioni 30 za ziada kwaajili ya kusimamia shughuli za kuweka usalama na ulinzi wa maeneo mbali mbali ikiwemo ya Ibada. Miongoni mwa mambo mengine yatakayojadiliwa kwenye mkutano huo ni pamoja pia na suala linalohusu uhuru wa mipaka wa kuingia nchi moja hadi nyingine katika umoja huo, na mageuzi ya sera za uhamiaji na waomba hifadhi.