Borrell: Kuanzishwa kwa taifa la Palestina ni suluhu
21 Novemba 2023Matangazo
Borrell amefanya mkutano kwa njia ya video na mawaziri wa mambo ya nje kutoka nchi 27 za Umoja wa Ulaya baada ya kuizuru Mashariki ya Kati kwa mazungumzo juu ya mzozo kati ya Israel na kundi la Hamas.
Mwanadiplomasia huyo mkuu wa Umoja wa Ulaya ameeleza kuwa, amepata kile alichokiita "hitimisho la msingi la kisiasa" kufuatia mazungumzo yake katika eneo la Mashariki ya Kati.
Amesisitiza kuwa, Israel haifai kuchukua udhibiti wa Gaza baada ya mzozo wa sasa kumalizika na kwamba udhibiti wa eneo hili unapaswa kuwa mikononi mwa mamlaka ya Palestina.