1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mauritius yatangaza tarehe ya uchaguzi, yavunja Bunge

4 Oktoba 2024

Ikulu ya Mauritius imetangaza leo Ijumaa kwamba taifa hilo la kisiwa litafanya uchaguzi wa bunge mnamo Novemba 10 na kwamba bunge la sasa limevunjwa kuanzia leo.

https://p.dw.com/p/4lQUY
Visiwa vya Chagos, Mauritius.
Visiwa vya Chagos, Mauritius.

Tangazo kutoka Ofisi ya Rais Prithvirajsing Roopun limetolewa siku moja baada ya nchi hiyo kufikia mkataba wa kihistoria na Uingereza utakaorejesha udhibiti wa Mauritius kwenye visiwa vya Chagos.

Kulingana na kalenda ya uchaguzi, ilikuwa bunge livunjwe mwishoni mwa mwezi Novemba na kisha uchaguzi mpya kuitishwa, lakini haijfahamika ikiwa uamuzi huo wa kulivunja sasa umechochewa na mkataba kati ya Mauritius na Uingereza. 

Soma zaidi: Mauritius yataka mamlaka ya juu ya visiwa vyake vya Chagos

Kwa miaka kadhaa, Uingereza ilipuuza shinikizo la kimataifa la kuvirejesha visiwa vya Chaogso chini ya milki ya Mauritius kwa sababu nchi hiyo inamiliki kambi ya kijeshi ya pamoja na Marekani kwenye moja ya visiwa hivyo. 

Licha ya hatua hii ya kuvirejesha visiwa hivyo mikononi mwa taifa hilo la mashariki ya Afrika, bado Uingereza na Marekani zitaendelea kubakisha kambi hiyo ya kijeshi.