1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mauritius yataka mamlaka ya juu ya visiwa vyake vya Chagos

8 Februari 2022

Serikali ya Mauritius imetuma ujumbe wake kwenye visiwa vya Chagos kushinikiza madai ya umiliki wa visiwa hivyo vya Bahari ya Hindi vinavyokaliwa na Uingereza na vyenye kambi ya kijeshi ya Marekani.

https://p.dw.com/p/46gwY
Karte Chagos-Inseln DE

Hii ni mara ya kwanza kwa Mauritius kupeleka ujumbe wake kwenye visiwa hivyo vilivyo kusini mashariki mwa Afrika bila ya kuomba ruhusa ya Uingereza.

Waziri Mkuu wa Mauritius, Pravind Jugnauth, amesema kwenye taarifa yake kwamba hii ni hatua muhimu ya kuchukuwa haki na mamlaka ya visiwa hivyo.

Mnamo mwaka 2019, Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC ilitowa uamuzi kwamba Uingereza ilikuwa inavikalia visiwa hivyo kinyume na sheria, ambavyo ilisema ni miliki ya Mauritius.

Visiwa cha Chagos vilikuwa sehemu ya Mauritius hadi Uingereza ilipovitwaa kabla ya taifa hilo la mashariki mwa Afrika kupata uhuru wake mwaka 1968.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW