1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Matumaini yakoje katika kutano wa tabia nchi mjini Doha?

26 Novemba 2012

Mkutano wa 18 wa kimataifa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi umefunguliwa mjini Doha, bila ya kuwepo matumaini ya kufikiwa makubaliano ya kupunguza moshi wa viwandani.

https://p.dw.com/p/16pmb
Jengo la mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi mjini DohaPicha: cop18.qa

Miongoni mwa mada zitakazojadiliwa ni namna ya kufikiwa itifaki ya pili ya Kyoto ,kubuni njia ya kupatikana makubaliano jumla hadi ifikapo mwaka 2015 na kupatiwa misaada ya fedha nchi zinazokabiliwa na hatari zaidi ya kuathirika na mabadiliko ya tabia nchi.

Wataalam wanahofia ikiwa hatua hazitachukuliwa janga la joto mfano wa lile lililoshuhudiwa Urusi msimu wa kiangazi mwaka 2010 linaweza kuzuka upya,na kima cha maji ya bahari kikapanda huku mataifa yanayoinukia yakikabiliwa na balaa lisilo na mfano la ukame.

"Bila ya kuwajibika na kuchukua hatua zinazohitajika kupunguza moshi unaotoka viwandani, hali ya ujoto itaongezeka kwa nyuzi joto tatu ulimwenguni,ikilinganishwa na hali namna ilivyokuwa kabla ya enzi za viwanda.Hayo ni kwa mujibu wa ripoti iliyokabidhiwa benki kuu ya dunia na taasisi ya utafiti wa mabadiliko ya tabia nchi ya mjini Postdam nchini Ujerumani.

Dürre – Indien
Ukame nchini IndiaPicha: AP

Hata hivyo hakuna anaetegemea kama mkutano huu wa Doha utakaoendelea hadi December 7 ijayo,utapitisha hatua zozote za maana kusaidia kupunguza moshi wa viwandani.Sababu ya hayo anasema Sven Harmeling wa shirika la ulinzi wa mazingira linaloshughulikia sera za mabadiliko ya tabia nchi ulimwenguni "ni ile hali kwamba mengi yameshatangazwa katika mikutano iliopita na nchi nyingi kurekebisha sheria zao, kwa hivyo itakuwa shida kusema kama nchi hizo zitatoa ahadi yoyote ikiwa hazina hakika kama malengo yaliyowekwa hadi sasa yatafikiwa."

Baadhi ya mataifa yanayoinukia yanategemea kupatiwa ahadi anaendelea kusema Sven Harmeling:"Kuna zaidi ya nchi 100 ambazo bado hazijatamka lolote kuhusu hatua za kupambana na mabadiliko ya tabia nchi,miongoni mwa nchi hizo,zinakutikana pia Philippines,Thailand,na pia nchi za kiarabu,mfano Saud Arabia na Qatar.

Erderwärmung Gletscher schmilzt
Joto linasababisha milima ya theluji kuyayuka GreenlandPicha: picture alliance/WILDLIFE

Ufanisi au kushindwqa mkutano wa Doha kutategemea kama maridhiano yatafikiwa ya kurefusha itifaki ya Kyoto.Nchi za Umoja wa Ulaya zinataka muda wa itifaki hiyo ambao utamalizika mwishoni mwa mwaka huu,urefushwe hadi mwishoni mwa mwaka 2020 ambapo mataifa yanayoinukia yatawajibika nayo pia kupunguza moshi wa viwandani.Lakini wawakilishi wa mataifa mengine,wanapendelea itifaki ya Kyoto irefushwe kwa miaka mitano badala ya minane.

Mwandishi: Rönsberg,Andrea/Hamidou Oummilkheir

Mhariri: Mohammed Khelef