1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mataifa yatakiwa kuchukua juhudi zaidi kupunguza gesi zinazoharibu mazingira.

9 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CZGm

Bali, Indonesia. Pendekezo la muswada katika mkutano wa umoja wa mataifa unaohusika na mabadiliko ya hali ya hewa katika kisiwa cha Bali limeyataka mataifa yote kuchukua juhudi zaidi kuweza kuzuwia athari kubwa zaidi za mabadiliko ya hali ya hewa. Pendekezo hilo la muswada lililoandikwa na wajumbe kutoka Indonesia , Australia na Afrika kusini , linasema kuwa juhudi za hivi sasa hazitafanikiwa upunguzaji wa utoaji wa gesi unaohitajika.

Mazungumzo hayo ya mabadiliko ya hali ya hewa yanayoyaweka pamoja mataifa 190 yanataka kutayarisha njia ya kupatikana makubaliano mapya yatakayochukua nafasi ya mkataba wa Kyoto, ambao unamalizika muda wake 2012. Mtayarishaji wa mkutano huo Yvo de Boer amesema kuwa majadiliano kuhusiana na makubaliano mapya yanaendelea vizuri. Lakini Marekani imeonyesha kuwa inakataa ulazima wa kupunguza kwa lazima kimataifa gesi zinazoharibu mazingira. Marekani haijatia saini makubaliano ya Kyoto.