1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afrika kupata mashine 300 ya kupumua kutoka wakfu wa Jack Ma

23 Aprili 2020

Wakfu wa bilionea wa Kichina Jack Ma umetoa msaada wa mashine 300 za kusaidia upumuaji kwa ajili ya mataifa ya Afrika yanayokabiliwa na uhaba wa mashine hizo muhimu katika matibabu ya ugonjwa wa covid-19.

https://p.dw.com/p/3bK2T
Rwanda Kigali | Beatmungsgeräte | Manufaktur in Kigali
Picha: DW/S. Karemera

Mkurungenzi wa vituo vya kuzuwia magonjwa barani Afrika CDC John Nkengason, alisema wiki iliyopita kwamba mataifa kumi ya Afrika ambayo hakuyataja yalikuwa yanalikabili janga hilo pasipokuwa na mashine hata moja ya kupumua.

Nkengason ameuambia mkutano wa waandishi habari kuwa mataifa hayo yatapewa kipaumbele katika ugawaji wa mashine hizo, ambazo amesema zitawasili katika wiki zijazo.

Mabilionea wa Kichina na mwasisi wa kampuni ya biashara ya mtandaoni ya Alibaba, ametoa pia msaada wa maelfu ya vifaa vya upimaji wa virusi vya corona, barakoa na vifaakinga kwa mataifa ya Afrika.