SiasaSudan
Marekani yaweka vikwazo vipya dhidi ya taasisi za Sudan
1 Juni 2023Matangazo
Mapema leo, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken alikuwa ameonya kwamba nchi yake inaweza kuwachukulia hatua viongozi wa makundi yanayopigana nchini Sudan baada ya kuvunjika kwa makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyosimamiwa na Marekani na Saudi Arabia.
Mwanadiplomasia huyo wa Marekani hakubainisha wazi ikiwa hatua hizo zitawalenga majenerali wanaoongoza makundi hasimu katika mzozo wa Sudan.
Wakati huo huo duru kutoka Sudan zimearifu kuwa watu 18 wameuawa katika shambulizi la anga lililolipiga soko moja mjini Khartoum leo Alhamisi. Na Umoja wa Mataifa umesema kuwa idadi ya raia wa Sudan waliokimbilia nchini Chad imepindukia watu 100,000.