Marekani yapinga azimio la UN la usitishaji mapigano Gaza
21 Novemba 2024Marekani ndio mwanachama pekee wa Baraza la Usalama aliyepiga kura ya kupinga mswada huo. Wanachama wengine 14 - wakiwemo washirika wa Marekani ambao ni Uingereza na Ufaransa - waliuunga mkono.
Soma pia: Wapalestina 15 wauawa na jeshi la Israel huko Gaza
Mwakilishi wa Marekani alikosoa mpango huo kwa kutoungaisha usitishwaji mapigano na kuwachiwa kwa mateka wa Israel. Rasimu hiyo iliyowasilishwa na wanachama 10 wasio wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama ilitoa wito wa kusitishwa mara moja kwa mapigano na kuwachiliwa mara moja na bila mashariki kwa mateka wote ambao bado wanashikiliwa na Hamas.
Hata hivyo, haikuyaunganisha matukio hayo mawili. Balozi wa Israel kwenye Umoja wa Mataifa alilitaja azimio hilo lililopendekezwa kuwa "la usaliti." Wakati huo huo, wizara ya Afya inayoendeleshwa na Hamas huko Gaza inesema idadi ya vifo katika ukanda huo inakaribia watu 44,000.