Rais Joe Biden wa Marekani amebadilisha uamuzi wa mwaka 2020 wa mtangulizi wake, Donald Trump, wa kuwaondoa wanajeshi wa Marekani kutoka Somalia. Marekani sasa itapeleka wanajeshi wake 500 huko. Je, hatua hii ina uhusiano na kuchaguliwa kwa rais mpya wa Somalia, na athari zake ni zipi? Daniel Gakuba amezungumza na Prof. Peter Kagwanja, mchambuzi wa masuala ya Upembe wa Afrika