1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mamilioni wapinga marekebisho ya malipo ya uzeeni Ufaransa

8 Machi 2023

Zaidi ya watu milioni moja nchini Ufaransa wamejitokeza katika mitaa ya Ufaransa kuandamana dhidi ya pendekezo la serikali la kufanyia marekebisho sheria za malipo ya uzeeni.

https://p.dw.com/p/4ONjn
Frankreich Paris Protest gegen Rentenreform
Picha: Lewis Joly/AP Photo/picture alliance

Zaidi ya watu milioni moja nchini Ufaransa wamejitokeza katika mitaa ya Ufaransa kuandamana dhidi ya pendekezo la serikali la kufanyia marekebisho sheria za malipo ya uzeeni.

Inaripotiwa kwamba wafanyakazi milioni 3.5 wamejitokeza na kuandamana huku maandamano hayo yakitajwa kuwa makubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa dhidi ya pendekezo hilo la Rais Emmanuel Macron na yanafanyika wakati ambapo bunge la seneti la Ufaransa linajadili pendekezo hilo.

Kulingana na muungano wa wafanyakazi, CGT, baadhi ya safari za ndege zilifutiliwa mbali na usambazaji wa mafuta ulisitishwa katika viwanda vyote vya kusafishia mafuta nchini humo. Serikali ya Rais Macron inataka kuongeza kiwango cha pesa kinachotolewa na wafanyakazi kwa ajili ya malipo ya uzeeni.