Maelfu ya watu waandamana Georgia kupinga uchaguzi wa bunge
29 Oktoba 2024Hayo ni wakati upinzani ukitoa miito ya kurudiwa uchaguzi huo chini ya uangalizi wa kimataifa. Rais anayeegemea nchi za Magharibi, Salome Zourabichvili, aliwahutubia waandamanaji, huku watu wakipeperusha bendera za Ulaya na Georgia mbele ya bunge.
Rais alisema hatoyatambua matokeo ya uchaguzi wa Jumamosi kwa sababu yalichakachuliwa na kuwa dosari nyingi zilitokana na uingiliaji wa Urusi. Licha ya ushahidi wa kutosha wa dosari, tume ya uchaguzi ya Georgia ilikitangaza chama tawala cha kihafidhina cha siasa za kizalendo Georgian Dream kuwa mshindi kwa asilimia 54 ya kura.
Soma pia: Upinzani nchini Georgia waitisha maandamano kupinga matokeo ya uchaguzi wa bunge
Miungano ya upInzani inayoegemea Ulaya ilipata asilimia 11 ya kura. Urusi imesema haikuingilia katika uchaguzi huo. Msemaji wa Ikulu ya Kremlin Dmitry Peskov amesema madai hayo hayana ushahidi. Kremlin inautuhumu upinzani kujaribu kuidhoofisha nchi na kusema uingiliaji wowote hakutoka "upande wa Urusi."