1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaGeorgia

Upinzani nchini Georgia waitisha maandamano

28 Oktoba 2024

Upinzani nchini Georgia umeitisha maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi huku Umoja wa Ulaya ukitaka uchunguzi ufanyike juu ya dosari zilizojitokeza, kufuatia matokeo ya uchaguzi wa bunge yaliyoibuwa mvutano.

https://p.dw.com/p/4mIjg
Mwasisi wa Chama cha Georgian Dream cha nchini Georgia  Bidzina Ivanishvili
Mwasisi wa Chama cha Georgian Dream cha nchini Georgia Bidzina Ivanishvili akizungumza baada ya matokeo ya uchaguzi wa bunge kuanza kutangazwa. Oktoba 26, 2024 Picha: Irakli Gedenidze/REUTERS

Chama tawala kinachotuhumiwa kuegemea upande wa Urusi kimeshinda uchaguzi huo, ingawa Rais Salome Zurabishvili jana Jumapili aliituhumu Moscow kwa kuchochea udanganyifu kwenye uchaguzi huo.

Amesema kilichotokea ni operesheni maalum iliyoendeshwa na Urusi.

Kutokana na madai ya upinzani wenye hasira, Rais Zurabishvili na rais wa zamani aliyeko jela Mikheil Saakashvili wameitisha maandamano ya umma.

Umoja wa Ulaya ulionya kwamba uchaguzi uliofanyika unatazamwa kama mtihani wa kidemokrasia katika taifa hilo ambao huenda ukaamuwa uwezekano wa Tbilisi kujiunga na jumuiya hiyo.