1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Janga

Macron: Shambulio dhidi ya Sinagogi ni ugaidi

24 Agosti 2024

Rais wa Ufaransa Emmanual Macron ameliita shambulio dhidi ya Sinagogi lililofanywa kusini mwa nchi hiyo kuwa ni kitendo cha kigaidi, ambacho nchi yake yenye umoja itapambana nacho.

https://p.dw.com/p/4jswt
Emmanual Macron
Rais wa Ufaransa Emmanual MacronPicha: Ruffer/Caro/picture alliance

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X, Macron amesema, mapambano ya chuki dhidi ya Wayahudi yanaendelea na juhudi zote zitafanyika ili kuwapata waliohusika na tukio hilo. 

Rais huyo wa Ufaransa ameyasema hayo baada ya mlipuko kuripotiwa nje ya Sinagogi katika mji wa Pwani wa La Grande Motte. Taarifa zinasema afisa mmoja wa polisi amejeruhiwa kutokana na mlipuko huo. 

Ufaransa: Mshirika wa mshambulizi wa Nice atiwa mbaroni

Ofisi ya Mwendesha mashtaka yenye jukumu la kupambana na ugaidi imesema kuwa itachukua jukumu la uchunguzi wa tukio hilo. Awali kaimu Waziri Mkuu wa Ufaransa Gabriel Attal alisema kuwa, harakati za kumtafuta aliyehusika na shambulio hilo zinaendelea.