1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Machafuko yazuka Sweden baada ya kuchomwa kwa Quran

4 Septemba 2023

Polisi ya Sweden imefahamisha leo,kwamba machafuko yamezuka katika mji wa tatu kwa ukubwa nchini humo baada ya waandamanaji wanaowapinga waislamu kuteketeza kitabu cha Quran.

https://p.dw.com/p/4VusQ
Iran Demonstrationen im Iran gegen die Verbrennung des Korans
Baadhi ya waandamanaji wakichoma bendera ya Sweden baada ya kuchomwa kwa QuranPicha: Sobhan Farajvan/Pacific Press/picture alliance

Polisi katika mji wa Malmo wamesema walishambuliwa kwa mawe na magari kadhaa yameteketezwa moto ikiwemo magari yaliyoegeshwa katika gereji ya chini kwa chini.

Machafuko hayo yalianza jana Jumapili kwa mujibu wa polisi na yameendelea usiku kucha.

Soma pia:Sweden kuimarisha doria za mpakani kufuatia kuteketezwa kwa Qur'an

Yalizuka baada ya mwanaharakati anayepinga Uislamu Salwan Momika jana Jumapili kuteketeza nakala ya kitabu cha Quran na kundi la watu wenye hasira walijaribu kumzuia wakati kwa upande mwingine Polisi wakiwakamata watu chungunzima.

Kufikia leo asubuhi mapema,kundi la watu wenye ghadhabu,wengi vijana pia walitia moto matairi nakufanya uharibifu mwingine katika eneo la Rosegard kwenye mji huo wa Malmo.

Hivi karibuni Sweden imekuwa ikiandamwa na matukio ya namna hiyo yanayosababisha na kuchomwa kwa kitabu cha Quran.
 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW