LOS ANGELES: Mabadiliko ya hali ya hewa ni changamoto kubwa
13 Oktoba 2007Matangazo
Makamu wa zamani wa rais wa Marekani,Al Gore amesema,kutunukiwa Tuzo ya Amani ya Nobel ni heshima na ni nafasi ya kuwazindua walimwengu,juu ya hatari za ongezeko la joto duniani. Alipozungumza na waandishi wa habari mjini Palo Alto katika jimbo la California alisema, mabadiliko ya hali ya hewa,ni changamoto kubwa kabisa kupata kubaliwa na ulimwengu.Gore alikuwa akizungumza saa chache baada ya Halmashauri ya Nobel mjini Oslo kutangaza kuwa Gore atagawana Tuzo ya Amani na Jopo la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya mabadiliko ya hali ya hewa.
Kansela wa Ujerumani,Angela Merkel amesema,Tuzo ya Amani ya Nobel iliyotolewa kwa Gore na wenzake ni mchango muhimu kwa juhudi za kuhifadhi mazingira kote duniani.