Kupunguzwa ufadhili kwatishia elimu kwa wakimbizi Rwanda
20 Oktoba 2023Matangazo
Mwishoni mwa wiki iliyopita, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR) lilitangaza kupunguza ufadhili wa chakula, elimu, malazi na huduma za afya mnamo wakati matumaini ya kupata dola milioni 90.5 za ufadhili yakififia.
Msemaji wa UNHCR, Lilly Carlislex, amesema hadi sasa ni dola milioni 33 pekee ndizo zilizopatikana, na kuongeza kuwa shirika hilo haliwezi kutimiza mahitaji yote ya wakimbizi.
Rwanda inawahifadhi wakimbizi 134,519, wengi wao kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Burundi na mataifa mengine.