1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiRwanda

Muswada wa Uingereza kuhusu wahamiaji watarajiwa kuwa sheria

19 Julai 2023

Muswada wenye utata wa Uingereza kutaka kuwazuia wahamiaji wasio na vibali kuingia nchini humo, unatarajiwa kuwa sheria sasa. Umoja wa Mataifa umeikosoa hatua hiyo.

https://p.dw.com/p/4U6bB
Wahamiaji waota moto katika mpaka kati ya Marekani na Mexico mnamo Desemba 22, 2022 huko El Paso, Texas.
Wahamiaji waota moto katika mpaka kati ya Marekani na MexicoPicha: John Moore/Getty Images/AFP

Wapinzani wa muswada huo katika bunge la Uingereza walikuwa wanataka ulegezwe kidogo kwa kufanyiwa mabadiliko ila juhudi zao hazikufua dafu. Sasa muswada huo utakuwa sheria baada ya utaratibu wa Mfalme Charles wa tatu kuukubali.

Wahamiaji wasio na vibali kupelekwa katika nchi zengine kama Rwanda. 

Sheria hiyo itafanya kuwa kinyume cha sheria, maombi ya kutaka hifadhi ya wahamiaji wote wanaowasili nchini humo kupitia ujia wa bahari wa Uingereza na njia zengine zote haramu. Wahamiaji watakaoingia nchini humo kwa njia hizo sasa watapelekwa katika nchi zengine kama Rwanda. 

UNHCR yalaani hatua hiyo

Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu wakimbizi UNHCR limelaani hatua hiyo likisema huo ni ukiukaji wa sheria ya kimataifa na kutahadharisha kwamba, sheria hiyo itawaweka wakimbizi kwenye hatari kubwa.