Kupanda kwa kiwango cha Joto - Mabadiliko ya hali ya hewa
26 Februari 2010Ingawa si kosa lako, hali hii inaendelea kutuathiri kwa kiwango kikubwa. Bara la Afrika ndilo litakalo athirika zaidi na mabadiliko ya hali ya hewa, licha ya kwamba bara la Ulaya na Marekani ndiyo yanayochangia pakubwa ongezeko la kiwango cha gesi ya Kaboni na moshi angani – chanzo kikubwa cha ongezeko la kiwango cha joto duniani.
Ni bara la Afrika ambalo limo hatarini zaidi kwa sababu, bara hili hutegemea sana kilimo. Sehemu nyingi za bara hili zinakumbwa na ukame, mawimbi ya joto kali na misimu isiyoweza kutabirika, hivyo kuifanya vigumu kuendesha shughuli za kilimo cha aina yoyote.
Je ni vipi unaweza kushirikiana na wengine ulimenguni katika kampeni ya kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa kijijini mwako. Hilo ndilo swali wanalojiuliza Joshua, Carol, Lorna na Alex katika mchezo wa redio Noa Bongo jenga maisha yako kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa. Ni vijana wannne walioamua kuchukua hatua ya kupinga mradi wa ujenzi wa kiwanda cha umeme kijijini mwao, na mwishowe kujifunza mengi tu ya kushangaza kuhusiana na suala zima la mabadiliko ya hali ya hewa.
Vipindi vya “Learning by Ear” ‘Noa bongo Jenga Maisha yako; vinasikika katika lugha sita: Kiingereza, Kifaransa, Kiswahili, Hausa, Kireno na Amharic. Na vinafadhiliwa na wizara ya mambo ya nchi za kigeni ya Ujerumani.